POLISI NA WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA WAWEKA MIKAKATI YA KUONGEZA USHIRIKIANO

na radiofaraja

Waandishi wa habari na Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga, wamekubaliana kukuza ushirikiano na uhusiano, ili kuongeza ufanisi wa kazi  kwa pande hizo mbili, kwa ajili ya manufaa ya Wananchi.

Makubalino hayo ambayo yamefikiwa hii leo, ni mwendelezo wa mdahalo wa pamoja kati ya pande hizo mbili, ambao umeandaliwa na Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga, wenye lengo la kuimarisha ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari, wakati wanapotekeleza majukumu yao.

Kupitia mdahalo wa leo, Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga, wameliomba jeshi la Polisi kutowachukulia kama wahalifu, na badala yake litambue umuhimu wao katika kuhabarisha Umma, hivyo linapaswa kuwapa ushirikiano na kuhakikisha linawalinda wakati wa kutekeleza majukumu yao.

Kwa upande wake kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Kamishina msaidizi wa Polisi Leonard Nyandahu, amewakumbusha waandishi wa habari kufanya kazi zao kwa weledi, ili kuepuka migongano isiyokuwa ya lazima kati yao na vyombo vingine.

Kupitia Mdahalo wa leo, pande hizo mbili zimeunda kamati maalum itakayosimamia masuala ya uhusiano, ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari, ambapo Miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo kwa upande wa jeshi la Polisi ni Mkaguzi wa Polisi Patrick Mkude na Koplo Gabriel Kayaga.

Wajumbe wa kamati hiyo kwa Upande wa waandishi wa habari mkoa wa Shinyaga ni Karen Masasi, Malunde Kadama,Neema Sawaka na Marco Mipawa.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA SHINYANGA ACP LEONARD NYANDAHU
AKIZUNGUMZA KWENYE MDAHALO
MWENYEKITI WA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SHINYANGA
GREYSON KAKURU
AKIZUNGUMZA KWENYE MDAHALO
MENEJA VIPINDI MSAIDIZI NA MHARIRI MKUU RADIO FARAJA SIMEO MAKOBA
AKICHANGIA MADA KWENYE MDAHALO
BAADHI YA MAAFISA WA JESHI LA POLISI WAKIWA KWENYE MDAHALO
BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI WAKIFUATILIA MDAHALO
Please Share This

Related Posts

Acha maoni