ASKOFU SANGU AWATAKA WATANZANIA KUKATAA NDOA ZA JINSIA MOJA, ZINAVURUGA MFUMO MZIMA WA FAMILIA NA JAMII

na radiofaraja

Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, ameendelea kuwatahadharisha Watanzania, kuwa makini na suala la ndoa za jinsia moja, ambazo amezitaja kuwa zinavuruga mfumo mzima wa familia.

Askofu Sangu ametoa rai hiyo leo, wakati akizungumza na waamini wa Parokia ya Chamugasa iliyopo wilayani Busega mkoani Simiyu,ambako yuko kwa ziara yake ya kichungaji ya siku mbili.

Amesema endapo Watanzania wataendekeza starehe na kupokea jambo hilo, mfumo wote wa jamii utavurugika, kwa kuwa ndoa ya Mume na Mke pekee ndiyo chanzo cha familia, ikiwemo miito ya Upadre na Utawa.

SAUTI YA ASKOFU SANGU

Wakati huohuo, Askofu Sangu amewaasa wanandoa kuongozwa na karama ya uvumilivu, pamoja na kuwa makini na watu wenye nia ya mbaya ya kuvuruga ndoa zao, na hasa watu wa karibu, kutoka pande zote za wanandoa.

SAUTI YA ASKOFU SANGU

Akiwa katika Parokia hiyo ya Chamugasa, Askofu Sangu amefungisha ndoa mbili na kuwaimarisha Wakristo wapya wapatao 77, ambao wanatoka katika Senta mbili za Parokia hiyo za Nyamikoma na Chamugasa.

Askofu Sangu akipokelewa kwa shangwe na Waamini mara baada ya kuwasili katika Parokia ya Chamugasa
Askofu Sangu akitoa Sakramenti ya Kipaimara
Askofu Sangu akifungisha ndoa
Maharusi wakisaini cheti cha Ndoa
Baadhi ya waamini wa Parokia ya Chamugasa wakifuatilia adhimisho la Misa
Paroko wa Parokia ya Chamuga Padre Dustan Sitta akitoa neno la shukrani
Askofu Sangu akitoa baraka kwa waamini
Please Share This

Related Posts

Acha maoni